Thursday, June 25, 2015

Belle 9 aeleza sababu zinazokwamisha muziki wake kufika Kimataifa


Belle 9 ni msanii anaefanya vizuri sana Local kuliko kimataifa kama walivyo wasanii wengine alioanza nao pamoja.













Belle 9 amezitaja sababu kubwa mbili ambazo zinamkwamisha kuianza safari yake ya kwenda kimataifa;
Kwa mimi binafsi nahisi ni connection ndo kitu ambacho ninakosa, na pia management ambayo iko serious kwasababu nimekuwa kwenye management kipindi cha Sumu ya Penzi, Masogange, toka We ni Wangu mpaka leo hii still niko mwenyewe naendelea kufanya hustle mwenyewe, kwahiyo ni tofauti na wasanii wengine ambao wanausimamizi , yaani sijapata serious management nimekuwa tu na ma agent tu wengi , pia niko na timu yangu kama Belle 9 lakini management serious ambayo inaweza kufanya kazi serious bado sijaipata na ndio kitu naamini kinanichelewesha.
#chafujo

No comments:

Post a Comment