Friday, June 26, 2015

Tunda Man Katika Mipango ya Kuacha Bongo Fleva na kuimba Dini Tu.

Tunda Man ana mpango wa kuacha Bongo Fleva na kuingia Rasmi katika Kuimba Muziki wa Dili ya Kiislam maarufu kama Qaswida.

Akiongea katika kipindi cha XXL 255 ya Clouds Fm Tuna Man amesema atamalizia muziki wake katika kuimba muziki wa Dini. Tunda Man amesema "idea ya kufanya qaswida ilikuwa katika plan yangu na ninafikiria muziki wangu unaweza kuishia huko, muziki wangu utaishia katika kuimba nyimbo za dini tu, yan itafikia huko yan, kwa hiyo naanza kabisa kufanya hizi ngoma kwa sababu baadae inaweza kunirahisishia kwa sababu muziki wangu natamani uweze kuishia kwenye kuimba Qaswida katika kumsifia Mwenyezi Mungu na Mitume wake, itakuwa ndo hivyo yan ntakuwa siimbi sana Dunia nafkiri ni mwanzo mzuri kila baada ya mwezi wa ramadhani nafanya hivyo halafu baadae ntakuja kila baada ya mwezi wa shaaban ntakuwa nafanya sana Qaswida, hivyohivyo baadae ntaenda straight kwa Mungu ambapo sitaimba tena nyimbo za Dunia".
#chafujo

No comments:

Post a Comment